IQNA

Harakati za Qur'ani

Msomi: Mafundisho ya Qur’ani  yanaweza kutusaidia kuondoa mfadhaiko

21:04 - August 06, 2024
Habari ID: 3479236
IQNA - Mwanazuoni wa Pakistan amezungumza kuhusu nafasi ambayo mafundisho ya Qur'ani Tukufu yanaweza kuchukua katika kukabiliana na mfadhaiko na wasiwasi.

Mafundisho ya Qur’ani Tukufu  yanaweza kutusaidia kuondoa wasiwasi na matatizo mengine ya kijamii, alisema Prof. Iqrar Ahmad Khan, Makamu Chansela (VC) Chuo Kikuu cha Kilimo Faisalabad (UAF).

Akihutubia hafla ya ugawaji wa Qur'ani iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkufunzi Mwandamizi UAF kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Bahauddin Zakariya, Multan, huko Faisalabad siku ya Jumatatu, alisema kwamba jamii bora inaweza kuanzishwa tu kwa kuziangazia nyoyo kwa mwongozo wa Mwenyezi Mungu unaotolewa katika Qur'an na Sunnah.

Amesema, "Tunaweza kuboresha maisha yetu kwa kuendeleza ikhlasi katika kutekeleza majukumu yetu na mafundisho ya Kiislamu yanaweza kusaidia kupata mafanikio duniani na akhera." Kwa kufuata kanuni za zenye thamani ya juu za Qur’ani na Sunnah, sio tu maisha ya mtu bali jamii nzima inaweza kuelekea kwenye ustawi," aliongeza.

Dk. Muhammad Ali alisema kuwa mafundisho ya Kiislamu yanaleta mafanikio katika kila nyanja ya maisha. “Tunapaswa kuzingatia mafundisho ya Qur’ani Tukufu na nakala mlizopokea za Qur’ani katika tukio hili ziwe zinasomwa popote pale muda utakapopatikana,” aliongeza.

Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Matibabu cha Nishtar, Shabbir Ahmad Nasir, Dk. Abdul Quddus, Mkufunzi Mwandamizi Dk. Shaukat Ali na wengine pia walizungumza katika hafla hiyo.

3489400

Habari zinazohusiana
captcha